Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha “Almuntaswar” kilikuwa chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, kimesambaza picha za Kanisa lilioungua hivi karibuni mjini Pari, ambapo chini yake wakaandika, subirini tukio la pili baada ya hili.
Vyombo vya usalama cha kupambana na ugaidi ambacho kilikuwa kikitangaza taarifa za uwezekano wa magaidi kushambulia nchini humo, wametangaza kuwa vitisho vya magaidi hao vinaashiria kuwa wao ndio waliosababisha kuungua kwa Kanisa Kubwa la Paris na kusema kwao “tusubiri tukio la pili” inaonyesha wanataka kufanya tukio lingi la kuunguza kanila lingine.
Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Ufaransa wametangaza kuwa moto uliounguza Kanisa hakuna mtu alisababisha tukio hilo, huku wakisisitiza kuwa tukio hili limetokea kwa kuungana nyaya za umeme, ambapo kwa upande mwengine maneno ya kikundi cha Almuntaswar hayaamanishi kuwa ndio waliohusika na kufanya tukio hilo.
mwisho/290
20 Aprili 2019 - 15:27
News ID: 937688

Kikundi cha kigaidi kilichokuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh kimesambaza picha za kutishia kuchoma moto makani ulimwenguni